MASWALI TISA AMBAYO HUPASWI KUJIULIZA TENA, UNAPOFANYA MALIPO KWA KUTUMIA MFUMO MPYA WA ARIS!!!

Campus Admin 2018-11-05 03:24:23 Notice Board

Hello Watumiaji wa mfumo huu mpya wa malipo bado wanajiuliza maswali kadhaa juu ya mfumo huu, leo tumekusogezea maswali tisa na majibu yake: 1. Mimi ninakidai chuo, kwa hiyo kwa huu mfumo mpya mimi nitasaidiwaje??. Jibu: Usihangaike, kama unakidai chuo nenda moja kwa moja kwa bursar wa chuo pale utawala mweleze shida yako, akiangalia kwenye system akaona ni sawa, anaweza kukusaidia kukamilisha malipo hayo. 2. Je nikishamaliza kulipa kwa mfumo huu, nina haja ya kufanya usajili tena??* Jibu: Ndio ni lazima ufanye usajili, utajaza form kama kawaida lakini ukifika college kufanya usajili wataangalia kwenye system ya Aris kudhibitisha kama umelipa, kama ushalipa unasajiliwa kama kawaida na unasubiri Kitambulisho chako. 3.Nini kitadhibitisha kuwa nimefanya malipo tiyari??. Jibu: Mambo mengi yatadhibitisha kuwa umefanya malipo, mfano Aris yako itaonesha umelipa kwa sababu ukishatiki malipo yako, taarifa zitatunzwa huko Aris, Pia utatumiwa meseji na mtandao ambao utafanyia malipo,mfano MPESA, TigoPesa na AirtelMoney.....kwa hiyo unaweza kuzitunza meseji hizo pia. 4. Je ni hiari au lazima kwangu kutumia mfumo huu??. Jibu: Ni lazima kwa kila mwanafunzi wa UDSM kufanya malipo yake kwa kutumia mfumo huu mpya, ila kwa wale ambao walishafanya malipo kabla ya mfumo huu kuanza kutumika hao hawatasumbuliwa pia. 5. Mimi ni mwaka wa kwanza, sijui kitu kuhusiana na mfumo huu.Je nami napaswa kuutumia??. Jibu_: Ndio ni lazima kuutumia mfumo huu maana ukiingia Aris ... Username ni namba yako ya Usajili na password yako ya kuingilia ARIS ni Surname yako. 6. Je kama nataka kwenda kwa warden kupata chumba cha kulala, ntapeleka nini cha kudhibitisha nimelipia accommodation??. Jibu: Usihangaike, ukishafanya malipo taarifa zako zinatunzwa kwenye sytem, hivyo warden ana uwezo wa kuingia kwenye system na kuona endapo umelipa au hujalipia chumba. 7. Je kama sitaki kulipia kwa njia ya mtandao wa simu, labda nataka kutumia benki nifanyeje? Jibu_: Ni rahisi, ukishapewa control number kutoka ARIS, namba hiyo unaitumia kufanya malipo hata ukienda benki pia. 8. Je mbona kila nikitaka kujisajili kwenye mwaka wa masomo mpya naambiwa mpaka nilipe?. Jibu_: Ndio, huwezi kusajili mwaka mpya wa masomo mpaka ulipie malipo yote yanayohitajika. 9 Je nikihitaji msaada zaidi nifanyeje?. Jibu_: Usipate tabu kabisaa.. wasiliana na viongozi wako wa College, kama Mwenyekiti, Katibu, Excoms, na wabunge watakusaidia bila tatizo. Ahsanteni. Imetolewa na DARUSO-CoSS